Friday, January 28, 2011

Angalia Hii!

Soma kwa makini, Kisha utafakari.
Ni magumu mangapi umekuwa ukiyapitia au kukutana nayo maishani mwako?
Umewahi kujiuliza ni wangapi pia hupitia magumu kama wewe? Bila shaka
tena zaidi kuliko yako. Tumekuwa watu wa kulaumu na kumwambia Mungu. "God Why Me?"
Hebu tafakari na uangalie video ya kijana huyu. Kisha ikutie moyo na kukufanya
usiwe mtu wa kukata tamaa kirahisi maishani. Ukishindwa mtihani usione kama ndio
mwisho wa maisha jaribu tena na tena. Hebu tafakari hili nalo. Inasemekana mtu aliyetengeneza bulb (taa ya umeme au gropu) Alikuwa anajaribu kutengeneza akirudia mpaka mara elfu moja ndo akafanikiwa kuitengeneza na sasa inakuwezesha kupata mwanga wakati wa giza. Ndugu yangu usiwe mtu wa kukata tamaa kirahisi. Jaribu tena na tena.
Zaburi 55:22 "Umtwike Bwana mzigo wako naye atakutegemeza, Hatamwacha mwenye haki aondoshwe milele."

Thursday, January 13, 2011

Kijitonyama Youth Familialization Day

Siku ilianza kwa vijana kuutafuta uwepo wa Mungu kwanza kabla ya mambo yote.

Kama wanavyoonekana wakiimba katika roho. Wakiimba nyimbo za kuabudu kabla maombi ya kuwatangulia hayajaanza.
Wakimtafakari Mungu Kama wanavyoonekana kwenye picha wakiwa kanisani

Baada ya kuwa wamewasili katika Hotel ya Kunduchi Beach Hotel upande wa Wet n Wild Wakiingia kwa umati kama picha inavyoonesha

Mazoezi yalichukua nafasi yake kabla semina hazijaanza

Hawa ni vijana wa umri wa kuanzia kipaimara na wale wa o-level. Wakiongozwa na mwalimu wao wa mazoezi Bw. Siaoforo Kishimbo (mwenye suruali ya rangu nyekundu)

Hapa ni vuta nikuvute vijana wanaimarisha viungo na kujenga afya zao kwa kufanya mazoezi

Bwana Gerald John a.k.a BIG akitoa huduma ya kwanza

Huu ni upande wa 26yrs and above wakiwa kwenye mazoezi pia

Mazoezi yaliwafanya wafurahie uwepo wao maeneo hayo

Ili mradi tu. Wengine hali wameweka miguu yao kwenye maji  huku wakisikiliza matangazo kama wanavyoonekana kwenye picha

Kweli walijitahidi kuwepo kwa wingi, wengine wakiwa wamesimama wengine wamekaa

Hili nalo lilikuwa ni moja ya pozi kila mtu kwa style yake

Bwana Lenard Shayo akitoa maelekezo kwa vijana waliokuwepo

Pembeni mwa Bw. Lenard Shayo ni 
Mchungaji wa usharika wa Kijitonyama Mch. Charles Mzinga
Alikuwepo pia kuhakikisha vijana wake wako salama 
na ratiba yao inaenda vizuri

Mwenye Bag Jeusi ni Mch. Lewis Hiza naye alikuwepo. 
Siwajua wito wake kwa vijana!

Tunapoza miguu kidogo jamani!

Pale wachungaji wanapokutana na kutambulishana. Basi mambo yalikuwa hivi!

Mch. Charles Mzinga akiwatambulisha watumishi ambao walihudumu katika kuendesha semina kwa vijana. 
mwenye shati jeusi ni Chriss Mauki, Akifuatiwa na Mch. Lewis Hiza

Praise and Worship Team ya siku hiyo wakiimba

Mwalimu Mgisa Mtebe naye hakukosa, 
Ningeshangaa sana kama asingekuwepo!!
Vijana wakiufurahia uwepo wake. Kama anavyoonekana akifundisha
 
Wakiwa wanasikiliza kwa makini somo linalotolewa na Chris Mauki

Somo limekolea hakuna hata anayefunga kope

Mtumishi Mshana na Neema Munisi pia walikuwepo
 
Viongozi wa kamati ya maandalizi Bw. Ahaz Chali na Bw. Lenard Shayo wakiwa
busy kuhaki siku inaenda kama ilivyopangwa

Hawa nao ni viongozi. 
Walikuwa busy jamani kuhakikisha vijana wanafanikisha siku yao

Mch. Lewis Hiza akifundisha vijana kwa umakini

Vijana wakiwa busy kuchukua notes. wengine wanasikiliza

Hili ni tent ambalo moja ya semina ilifanyikia humo
 
Mchungaji akipewa progress ya ratiba nzima ya siku hiyo na mlezi wa vijana Mr. Lenard Shayo

Ni pozi tu la kupigia makofi

Ni warm up tu baada ya kukaa kwa muda mrefu baada ya semina

Ni warm up tu baada ya kukaa kwa muda mrefu baada ya semina

Michezo mbalimbali ilitawala. Huu wa mpira wa miguu ulikuwepo pia

Vijana wadogo ndio walionza kucheza baadae wakacheza na kaka zao. Hatimaye vijana wadogo. namaanisha wale wa umri kuanzia kipaimara na walio o-level wakawafunga kwa mikwaju wale wa 26 and above

Sogea uone!

Viongozi wa Kamati ya Maandalizi wakiwa Kazini

Kwenye picha ni viongozi wa kamati ya maandalizi ya siku ya familiarization wakiandaa mikakati mbalimbali ya nini kifanyike siku hiyo ya tarehe 12 January 2011.
 Tokea shoto ni Bw. Ahaz, Nia, Lee, Kishimbo, Judith, Anitha na Brenda

 Wakijiuliza nini kifanyike.

Bwana Michael Karata ambaye ndiye mwenyekiti wa umoja wa vijana akiwasikiliza wajumbe wa kamati wakichangia hoja
 Bw. Renard Shayo ambaye ni mzee mlezi wa umoja wa vijana wa KKKT Kijitonyama
akiwa ameweka sample ya t-shirts yenye maneno "Arise and Shine" ambazo vijana watazivaa siku hiyo
Bwana Ahaz akichukua notes za kikao

Monday, January 10, 2011

KKKT-Kijitonyama

Kama linavyoonekana kwenye picha
Ni Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Usharika wa Kijitonyama. Ambalo ndipo 
Vijana wenye vipaji mbali mbali wamejitokeza kwa lengo moja na kuamua kuunda umoja wao
ili kupitia huo wamjue Mungu. Lakini pia kubadilisha uzoefu wa vipaji mbalimbali walionao. Kupitia huo jamii ifaidike pia.
 

Karibu katika blog Ya Vijana wa Kijito

Tunapenda Kuwakaribisha vijana wote wa Usharika wa Kijitonyama. 
Katika Blog yetu.
Blog yetu bado iko kwenye matengenezo hivyo tunaomba ushauri wako wa nini kifanyike kiongezwe kitu gani na kipunguzwe kipi. 
Tafadhali tuma maoni yako kwenye email yetu hapa chini.
youthkijitoelct@gmail.com
Mungu awabariki sana.