Thursday, January 13, 2011

Kijitonyama Youth Familialization Day

Siku ilianza kwa vijana kuutafuta uwepo wa Mungu kwanza kabla ya mambo yote.

Kama wanavyoonekana wakiimba katika roho. Wakiimba nyimbo za kuabudu kabla maombi ya kuwatangulia hayajaanza.
Wakimtafakari Mungu Kama wanavyoonekana kwenye picha wakiwa kanisani

Baada ya kuwa wamewasili katika Hotel ya Kunduchi Beach Hotel upande wa Wet n Wild Wakiingia kwa umati kama picha inavyoonesha

Mazoezi yalichukua nafasi yake kabla semina hazijaanza

Hawa ni vijana wa umri wa kuanzia kipaimara na wale wa o-level. Wakiongozwa na mwalimu wao wa mazoezi Bw. Siaoforo Kishimbo (mwenye suruali ya rangu nyekundu)

Hapa ni vuta nikuvute vijana wanaimarisha viungo na kujenga afya zao kwa kufanya mazoezi

Bwana Gerald John a.k.a BIG akitoa huduma ya kwanza

Huu ni upande wa 26yrs and above wakiwa kwenye mazoezi pia

Mazoezi yaliwafanya wafurahie uwepo wao maeneo hayo

Ili mradi tu. Wengine hali wameweka miguu yao kwenye maji  huku wakisikiliza matangazo kama wanavyoonekana kwenye picha

Kweli walijitahidi kuwepo kwa wingi, wengine wakiwa wamesimama wengine wamekaa

Hili nalo lilikuwa ni moja ya pozi kila mtu kwa style yake

Bwana Lenard Shayo akitoa maelekezo kwa vijana waliokuwepo

Pembeni mwa Bw. Lenard Shayo ni 
Mchungaji wa usharika wa Kijitonyama Mch. Charles Mzinga
Alikuwepo pia kuhakikisha vijana wake wako salama 
na ratiba yao inaenda vizuri

Mwenye Bag Jeusi ni Mch. Lewis Hiza naye alikuwepo. 
Siwajua wito wake kwa vijana!

Tunapoza miguu kidogo jamani!

Pale wachungaji wanapokutana na kutambulishana. Basi mambo yalikuwa hivi!

Mch. Charles Mzinga akiwatambulisha watumishi ambao walihudumu katika kuendesha semina kwa vijana. 
mwenye shati jeusi ni Chriss Mauki, Akifuatiwa na Mch. Lewis Hiza

Praise and Worship Team ya siku hiyo wakiimba

Mwalimu Mgisa Mtebe naye hakukosa, 
Ningeshangaa sana kama asingekuwepo!!
Vijana wakiufurahia uwepo wake. Kama anavyoonekana akifundisha
 
Wakiwa wanasikiliza kwa makini somo linalotolewa na Chris Mauki

Somo limekolea hakuna hata anayefunga kope

Mtumishi Mshana na Neema Munisi pia walikuwepo
 
Viongozi wa kamati ya maandalizi Bw. Ahaz Chali na Bw. Lenard Shayo wakiwa
busy kuhaki siku inaenda kama ilivyopangwa

Hawa nao ni viongozi. 
Walikuwa busy jamani kuhakikisha vijana wanafanikisha siku yao

Mch. Lewis Hiza akifundisha vijana kwa umakini

Vijana wakiwa busy kuchukua notes. wengine wanasikiliza

Hili ni tent ambalo moja ya semina ilifanyikia humo
 
Mchungaji akipewa progress ya ratiba nzima ya siku hiyo na mlezi wa vijana Mr. Lenard Shayo

Ni pozi tu la kupigia makofi

Ni warm up tu baada ya kukaa kwa muda mrefu baada ya semina

Ni warm up tu baada ya kukaa kwa muda mrefu baada ya semina

Michezo mbalimbali ilitawala. Huu wa mpira wa miguu ulikuwepo pia

Vijana wadogo ndio walionza kucheza baadae wakacheza na kaka zao. Hatimaye vijana wadogo. namaanisha wale wa umri kuanzia kipaimara na walio o-level wakawafunga kwa mikwaju wale wa 26 and above

Sogea uone!

1 comment:

  1. Mungu awe nanyi daima!!nimewamissi sana natumaini kwa mapenzi ya Mungu nitawaona tena!.

    ReplyDelete