Friday, January 28, 2011

Angalia Hii!

Soma kwa makini, Kisha utafakari.
Ni magumu mangapi umekuwa ukiyapitia au kukutana nayo maishani mwako?
Umewahi kujiuliza ni wangapi pia hupitia magumu kama wewe? Bila shaka
tena zaidi kuliko yako. Tumekuwa watu wa kulaumu na kumwambia Mungu. "God Why Me?"
Hebu tafakari na uangalie video ya kijana huyu. Kisha ikutie moyo na kukufanya
usiwe mtu wa kukata tamaa kirahisi maishani. Ukishindwa mtihani usione kama ndio
mwisho wa maisha jaribu tena na tena. Hebu tafakari hili nalo. Inasemekana mtu aliyetengeneza bulb (taa ya umeme au gropu) Alikuwa anajaribu kutengeneza akirudia mpaka mara elfu moja ndo akafanikiwa kuitengeneza na sasa inakuwezesha kupata mwanga wakati wa giza. Ndugu yangu usiwe mtu wa kukata tamaa kirahisi. Jaribu tena na tena.
Zaburi 55:22 "Umtwike Bwana mzigo wako naye atakutegemeza, Hatamwacha mwenye haki aondoshwe milele."

No comments:

Post a Comment